Penati ya Harry Kane ilitosha
kuifanya Uingereza kumaliza kampeni za kuwania kutinga fainali za
kombe la dunia kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Lithuania.
Mshambuliaji huyo wa Tottenham Kane
aliipatia Uingereza goli hilo pekee katika dakika ya 27 baada ya Dele
Alli kuchezewa rafu.
Kocha wa Uingereza Gareth Southgate
alifanya mabadiliko katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja
uliojaa maji ya mvua kwa kumuingiza Harry Winks na Harry Maguire.
Harry Kane akifunga goli pekee kwa mpira wa penati katika mchezo huo


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni