Timu ya Huddersfield Town imemaliza
rekodi ya Manchester United ya kutofungwa katika Ligi Kuu ya
Uingereza msimu huu kwa kuipa kipigo cha kwanza cha magoli 2-1.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye
dimba la John Smith's Manchester United walifungwa goli la kwanza
baada ya Juan Mata kupoteza mpira ulionaswa na Aaron Mooy.
Mooy aliambaa na mpira huo na
kumpasia kiungo Tom Ince aliyepiga mpira uliookolewa na kipa David de
Gea, na mpira huo kumkuta Mooy akaupachika wavuni.
Uzembe wa beki Victor Lindelof
uliizawadia Huddersfiel goli la pili lililofungwa na Laurent
Depoitre, huku Marcus Rashford aliyetokea benchi akifunga goli pekee
la Manchester United.
Laurent Depoitre akimzunguka kipa Davidi De Gea na kufunga goli la pili
Marcus Rashford akiuunganisha kwa kichwa mpira uliopigwa na Romelu Lukaku na kufunga goli pekee la Manchester United
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni