Ihembe walikuwa wa kwanza kupata goli dakika 25 kupitia kwa Athumani Chuji aliepiga shuti kali la mpira wa adhabu uliomshinda golikipa wa Nyaishozi na kuingia wavuni. Bao hilo lilionekana kuwachanganya Nyaishozi ambao walionyesha kutoelewana katika eneo la ulinzi na kujikuta wakiruhusu bao la pili katika dakika ya 35 lililofungwa na Mshauri Kato aliewatoka walinzi wa Nyaishozi na kufunga goli la kiustadi.
Kipindi cha pili Nyaishozi waliuanza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 78 lililofungwa na mshambuliaji MC, hata hivyo jitihada za kusawazisha matokeo zilikwamishwa na mlinda mlango wa Ihembe alieokoa michomo mingi.
Kufuatia ushindi huo Ihembe walijipatia kombe na kiasi cha fedha shilingi milioni moja na nusu huku Nyaishozi wakipata shilingi laki saba na nusu kama kifuta jasho kwa kushika nafasi ya pili. Akizungumza baada ya mchezo huo mbunge wa Karagwe Mheshimiwa Innocent Bashungwa alisema mashindano hayo yatakuwa endelevu kila mwaka ili kuibua vipaji vya vijana wa Karagwe waweze kujiajiri kupitia michezo na kuahidi kuboresha mashindano yajayo kwa kusaka wadau wengine watakaohakikisha wilaya ya Karagwe inakuwa na timu bora ya kushiriki ligi kuu.
Nae kocha bora wa ligi kuu msimu uliopita ambaye pia ni kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime aliyapongeza mashindano hayo na kuahidi mchezo wa kirafiki baina ya Kagera Sugar na kikosi cha wachezaji bora waliochaguliwa toka mashindano hayo.
Mbunge wa Karagwe Mheshimiwa Innocent Bashungwa akimpokea mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba
Mgeni rasmi akiwasili katika uwanja wa changarawe ilipofanyika fainali ya Bashungwa Karagwe Cup
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akikagua vikosi vya Ihembe na Nyaishozi
Mchezaji wa Ihembe akipiga mpira wa kona
Ihembe wakishangilia baada ya kupata bao la kwanza
Wachezaji wa Ihembe wakiwa wamemzunguka golikipa wao baada ya kupata kash kash
Mashabiki wa Nyaishozi wakifuatilia kwa makini mchezo wa Bashungwa Karagawe Cup
Kombe likikabidhiwa kwa mgeni rasmi
Mbunge wa Karagwe Mh. Innocent Bashungwa akitoa neno la pongezi kwa timu zote shiriki
Kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime akimkabidhi kombe nahodha wa Ihembe
Ihembe wakifurahia kombe lao la ubingwa wa Bashungwa Karagwe Cup
Furaha na shangwe baada ya kutangazwa mabingwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni