Msanii Kala Jeremiah akitumbuiza kwenye Kongamano la Uzinduzi wa Mabaraza ya Vijana Jijini Mwanza, lililofanyika uwanja wa Furahisha jumapili Oktoba 15,2017. Binagi Media Group
Kongamano hilo liliandaliwa na taasisi ya Youth & Environment Vision ya Jijini Mwanza kwa kushirikiana na taasisi ya Umoja wa Mataifa ya UNA Tanzania, The Foundation for Civil Society pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo Cocacola, TCRA, pepsi na Tecno.
Mgeni rasmi alikuwa Kaimu Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, William Mnyippembe ambaye aliwasisitiza vijana kujitambua kama ambavyo sera ya taifa ya vijana ya mwaka 2007 inavyosisitiza kwa kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo.
Aidha aliwataka kutumia vyema mitandao ya kijamii na kujiepusha na usambazaji wa jumbe zizizo na maadili katika jamii ikiwemo jumbe za uchochezi ambapo kongamano hilo liliwahusisha pia vijana kutoka shule mbalimbali Jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa taasisi ya Youth & Environment Vision, Jonathan Kassib alisema kongamano hilo lililenga kuwahamasisha vijana kuunda na kujiunga na mabaraza ya vijana katika mitaa yao kwa ajili ya utatuzi wa changamoto zinazowakabili ikiwemo kutumia fursa zinazowazunguka kupitia fedha za asilimia tano zinazotolewa na halmashauri kupitia mapato ya ndani.
Afisa Miradi kutoka UNA Tanzania, Saddam Khalfan alitoa wito kwa vijana kutilia maanani yale yanayopewa kipaumbele kupitia sera yao ya taifa kwa vijana na pia kuwa mstari wa mbele kujitafutia taarifa za kisera kwa ajili ya maendeleo yao.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mkolani wakitumbuiza kwenye kongamano hilo
Wanafunzi waliofanya vizuri kwenye michezo wakipokea zawadi kwenye kongamano hilo
Washindi wa michezo mbalimbali wakipokea zawadi kutoka kampuni ya simu ya Tecno
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni