Sergio Aguero ameifikia rekodi ya
mfungaji aliyeifungia Manchester City magoli mengi wakati Manchester
City ikiifunga Burnley magoli 3-0 na kuongoza ligi kwa tofauti ya
pointi tano.
Goli la Aguero la kipindi cha kwanza
alilofunga kwa penati iliyotolewa kwa utata limemfanya afikishe
magoli 177 kuifungia klabu hiyo sawa na mchezaji wa zamani wa
Manchester City Eric Brook.
Kocha wa Manchester City Pep
Guardiola alimkumbatia kwa furaha Aguero wakati mchezaji huyo wa
Argentina alipotoka uwanjani huku mashabiki wakisimama jukwaani
kuonyesha heshima kwake.
Sergio Aguero akifunga kwa kutulia mpira wa penati iliyotolewa kwa utata
Beki Nicolas Otamendi akifunga kwa kichwa mpira wa kona iliyopingwa na Kevin De Bruyne
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni