.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 2 Novemba 2017

ASKARI MAGEREZA KUTUKA WILAYA YA TEMEKE ASHINDA DAU KUBWA LA MILIONI 11O ZA TATU MZUKA

Afisa Magereza Bwana Neuro Mbwilo amejishindia dau kubwa kuwahi kutolewa na Tatu Mzuka la shilingi milioni 110 kupitia Mzuka jackpot iliyoonyeshwa kupitia vituo mbalimbali vya runinga nchi nzima siku ya Jumapili ya Tarehe 29 Nov 2017.

Kama ma milioni ya wachezaji wengine nchini Tanzania, Mbwilo alidhani ilikuwa ni fursa nzuri kutumia Shilingi 500 kubadilisha maisha yake pamoja na familia milele.

Bwana Mbwilo, ambaye ni Askari gereza wilayani Temeke alielezea mshtuko wake juu ya bahati iyo iliyomtembelea. "Ni hisia ambayo haielezeki kabisa. Nina furaha kubwa sana, nimejawa na shukrani nyingi,na kwangu hii ni ajabu kabisa ", alielezea mbele ya vyombo vya habari.

Katika kutoa hundi ya ushindi huo wa milioni 110 Bwana Sebastian Maganga, Meneja wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka alielezea zaidi juu ya ushindi huo mkubwa lakini aliwakumbusha Watanzania kwamba kuna njia nyingi za kushinda kupitia Tatu Mzuka. 

Alifafanua kuwa katika wiki 13 tu Tatu Mzuka imetengeneza zaidi ya washindi milioni 2 na kutoa billion 4 kwa washindi.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva ( Kushoto) akimkabidhi Mfano wahundi ya sh Milioni 110 Ofisa ya Jeshi la Magereza Neuro Mbwilo, ambaye
ni mshindi wa bahati nasibu ya Mzuka jackpot, Dar es Salaam.
Mshindi wa millioni 110 Bwn. Mbwilo akiwa na washkaji zake wawili Juma Athuman na Joseph Haule Walio zawadia milioni moja moja na Tatu Mzuka kwenye promotion ya "Cheza na Washkaji na Shinda na Washkaji".
Bwana Mbwilo akisherekea ushindi wake na Mke wake Nyumbani kwao Keko.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni