.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 4 Novemba 2017

BALOZI SEIF AIPONGEZA CUBA KWA KUSAIDIA MAENDELEO VISIWANI ZANZIBAR

Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Dmingo Herndez aliyesimama akizungumza katika Mkutano Maalum wa kuwaaga Madaktari Wazalendo wanoelekea Nchini Cuba kwa Mafunzo zaidi ya Udaktari Bingwa hapo katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar.

Kushoto ya Balozi Lucas Domingo ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bibi Halima Maulidi Salum akitoa shukrani za Wizara hiyo katika Mkutano wa kuaga Madaktari Wazalendo 15 kati yao Wanane wanaondoka hivi karibuni kuelekea Cuba kwa Masomo ua Udaktari Bingwa.
Balozi Seif Wanne kutoka Kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Wizara ya Afya, Balozi wa Cuba na Timu yake pamoja na Mataktari Wazalendo wanaojiandaa kuelekea Cuba kwa masomo ya juu ya Udaktari Bingwa mara baada ya kuwaaga rasmi Osifini kwake Vuga.
Balozi Seif kati kati akiwa pamoja na Uongozi wa Wizara ya Afya pamoja na Madaktari Wazalendo Wanane wanaotarajiwa kuondoka Nchini wakati wowote kuanzia sasakuelekea Cuba kwa mafunzo ya Udaktari Bingwa.

                                                                                  Picha na – OPMR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba juhudi zinazochukuwa na Serikali ya Cuba katika kuiunga Mkono Zanzibar kwenye Miradi ya Maendeleo hasa katika Sekta ya Afya imeanza kuleta mafanikio makubwa ya matumaini.

Alisema kitendo cha Cuba cha kukubali kuwagharamia Kimasomo Madaktari Wazalendo wa Zanzibar kufikia Utaalamu wa kuwa Madaktari Mabingwa ni mfano halisi wa matumaini hayo.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo mbele ya Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Hernadez Polledo katika Mkutano Maalum wa kuwaaga Madaktari Wazalendo 15 ambao Wanane kati yao wataondoka wakati wowote kuanzia sasa kuelekea nchini Cuba kwa Mafunzo zaidi ya Udaktari Bingwa.

Madaktari hao Wazalendo wa Zanzibar waliomaliza mafunzo yao kupitia mpango wa masomo ulioasisiwa kati ya Serikali ya Cuba na Zanzibar ni pamoja na Anas Mbarak Anas, Nihifadhi Issa Kassim, Rukia Abdulrahman Sadiq, Salama Makame Pandu, Said Simai Msalaka, Abdullah Omar Khamis, Yassin Khamis Moh’d na Mwadini Maalim Simai.

Balozi Seif alisema kundi la Pili laMadaktari hao Saba Wazalendo linatarajiwa kwenda Nchini Cuba Mwakani na kukamilisha Idadi ya Madaktari hao 15 kupitia uamuzi wa Cuba wa kukubali kusaidia Sekta hiyo kufuatia ziara ya hivi karibuni aliyoifanya Nchini Cuba kwa kukutana na Uongozi wa Wizara ya Afya pamoja na ile ya Mambo ya Nchi za Nje.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliendelea kuishukuru na kuipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Cuba kwa namna inavyoendelea kuunga mkono jitihada za Serikali zote mbili ile ya Zanzibar na ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaletea maendeleo Wananchi wake.

Mapema Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Hernadez Polledo alisema uhusiano wa kidoplomasia kati ya Cuba na Zanzibar ni wa Kihistoria kiasi kwamba, kupitia muingiliano wa mahusiano ya kubadilishana taaluma utaendelea kuimarika zaidi.

Balozi Lucas aliwakumbusha Madaktari hao wa Zanzibar kwamba Wananchi walio wengi wana matarajio ya kupata huduma za Afya zilizo makini kupitia Wataalamu wanaosomeshwa na Serikali kwa lengo la baadaye la kusaidia Jamii inayowazunguuka.

Alielezea matarajio yake kuiona Zanzibar ikijiwekea tayari kwa kuwekeza katika miundombinu ya Miradi mbali mbali ikiwemo sekta muhimu ya Afya ili kuleta matarajio kwa Wananchi pamoja na wageni wanaojipangia kutembelea Visiwa vya Zanzibar.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Wizara ya Afya Zanzibar Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Halima Maulidi Salum aliahidi kwamba Wizara ya Afya itaendelea kuwa karibu na Wahadhiri pamoja na Madaktari Bingwa kutoka Nchini Cuba wanaotoa mafunzo kwa Madaktari Wazalendo Visiwani Zanzibar.

Bibi Halima alisema nafasi zozote za kimasomo zitakazopatikana za kuongeza Taaluma kwa Madaktari na Watendaji wao, Wizara itajitahidi zaidi kuzichangamkia ili kuwajengea uwezo watendaji na Madaktari hao.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
4/11/2017.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni