Kiungo mshambuliaji Paul Pogba
amefunga goli akirejea dimbani kwa mara ya kwanza tangu aumie wakati
Manchester United ikitokea nyuma na kuifunga Newcastle United magoli
4-1 katika dimba la Old Trafford.
Katika mchezo huo Manchester United
ilijikuta ikitanguliwa kufungwa na wageni kupitia kwa Dwight Gayle
kutokana na kosa la beki Victor Lindelof, lakini hata hivyo Anthony
Martial alisawazisha goli hilo.
Beki Chris Smalling aliongeza goli
la pili alipoinasa krosi ya Ashley Young kabla ya mapumziko. Pogba
akafunga goli la tatu katika kipindi cha pili na kusaidia goli la nne
lililofunga na Romelu Lukaku.
Paul Pogba akimalizia kwa utulivu mpira uliopigwa na Marcus Rashford na kufunga goli la tatu
Romelu Lukaku akifunga goli la nne na kumaliza ukame wa kutofumania nyavu kwa muda katika Ligi Kuu ya Uingereza
Zlatan Ibrahimovic akifanya vitu vyake baada ya kucheza kwa dakika 14 kwa mara ya kwanza tangu aumie na kuwa nje ya uwanja kwa miezi saba
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni