.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 21 Novemba 2017

TENMET YAWASILISHA HOJA 14 KWA KAMATI YA BUNGE HUDUMA ZA JAMII

Na Mwandhishi Wetu, Dodoma

MTANDAO wa Elimu Tanzania (TENMET) umekutana na kamati ya Bunge Huduma za Jamii na Maendeleo na kuwasilisha hoja 14 ambazo wameiomba kuikumbusha Serikali kuzifanyia kazi ili kuboresha sekta ya elimu nchini.

Akiwasilisha hoja hizo mbele ya wajumbe wa kamati hiyo, mwishoni mwa wiki mjini Dodoma, mmoja wa wanachama wa TENMET kutoka ACTIONAID, Bw. Karoli Kadeghe aliiomba Serikali kutenga asilimia 20 ya bajeti ya taifa kwenye sekta ya elimu kama ilivyoahidi, kwani sasa badala ya bajeti kupanda imekuwa ikishuka na ndani ya miaka mitatu imepungua toka asilimia 17 hadi asilimia 15.

Alisema Serikali haina budi kuwekeza zaidi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato na matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kutoka vyanzo vya ndani ili viweze kutumika kufadhili elimu ya msingi na utoaji ruzuku shuleni uzingatieb hali halisi ya mahitaji ya sasa.

Bw. Kadeghe pia aliwaeleza wanakamati hiyo kuikumbusha Serikali juu ya kuanzisha mchakato wa Bodi ya Taaluma ya uwalimu itakayoongeza tija na kulinda maslahi ya walimu katika sekta ya elimu jambo ambalo kimekuwa kilio cha walimu kwa muda sasa.

Aliiomba Serikali kupitia kamati hiyo kuimarisha idara ya kudhibiti ubora (ukaguzi) na ipewe mamlaka na vitendea kazi kiuhalisia ili iweze kufanya kazi yake kiufasaha, kwani bajeti ya mwisho zilitengwa bilioni 42 ambazo hazikupelekwa hadi mwezi machi.

TENMET pia iliiomba Serikali kutoa kipaumbele cha bajeti kwa sekta ya elimu kama ilivyofanywa kwa sekta ya miundombinu miaka miwili iliyopita, na uzingatiwaji wa haki za watoto na kuundwa chombo maalumu cha usimamizi, utungaji na utekelezaji wa sera ya elimu.

Pamoja na hayo, Serikali za mitaa kutunga na kusimamia sheria ndogondogo zitakazo wabana wazazi wanaowanyima watoto haki ya elimu, huku wakiomba fedha za mikopo ya elimu ya juu bajeti kuongezwa na zitenganishwe na fedha za maendeleo ya wizara ya elimu, huku vigezo vya upatikanaji mikopo kupunguzwa.

Aidha ombi lingine ni kutaka kuhimarishwa kwa kamati za shule, kuhamashishwa upya kwa wazazi kuchangia maendeleo ya watoto wao kielimu, kuingiza kipengele cha elimu ya mlipa kodi katika mitaala ya elimu na pia serikali kupunguza vigezo katika upatikanaji wa mikopo ya elimu ya juu na kuongeza bajeti eneo hilo.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba aliwaahidi TENMET kuzifuatilia hoja 14 walizowasilisha wanachama wa TENMET ili ziweze kufanyiwa kazi hatua kwa hatua, ikiwa ni pamoja na kuwapongeza kwa uzalendo wanaouonesha kuipigania elimu nchini.

"...Kwa hiyo ndugu zangu niwaombe na niwahakikishie kama tulivyo kubaliana wakati ule...yale mambo 14 tutaendelea kuyasemea kama kamati, ili tuweze kuendelea kuboresha maendelea ni suala endelevu, sisi kama kamati tutaendelea kuiomba Serikali iwekeze fedha nyingi zaidi kwenye sekta hii ya elimu...maana hakuna mbadala wa elimu," alisema Peter Serukamba.

Kamati hiyo pia iliahidi kutembelea baadhi ya maeneo yenye changamoto kielimu kwa kukagua baadhi ya shule za msingi na sekondari kujionea changamoto na hali halisi ili kuendelea kuishawishi Serikali katika uboreshaji wa bajeti ya sekta ya elimu kiujumla.

Alitumia nafasi hiyo kuikumbusha jamii na hasa wazazi kutokwepa majukumu kwa watoto wao, kwani hakuna mtu anayeweza kujitokeza kazi yake ni kubeba majukumu ya mazazi/walezi kwa watoto wao. "...Lazima tusaidiane kuwakumbusha wazazi kutimiza majukumu yao, haiwezekani mzazi ukazaa alafu atokee mtu wa kutimiza majukumu yako.." alisisitiza mwenyekiti huyo.
Sehemu ya wabunge na wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii na Maendeleo wakichangia hoja katika kikao na TENMETkilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Sehemu ya wabunge na wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii na Maendeleo wakichangia hoja katika kikao na TENMETkilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wakichangia hoja mbalimbali katika kikao na wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii na Maendeleo kilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.

Baadhi ya wajumbe na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wakichangia hoja mbalimbali katika kikao na wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii na Maendeleo kilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wakichangia hoja mbalimbali katika kikao na wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii na Maendeleo kilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mwanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) kutoka taasisi ya ACTIONAID, Bw. Karoli Kadeghe (kushoto) akiwasilisha hoja 14 kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii na Maendeleo mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba akizungumza mara baada ya kupokea wasilisho la hoja 14 kutoka kwa wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), hoja hizo zililenga maboresho katika sekta ya elimu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni