Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo ambaye alikuwa ni mgeni rasmi akitoa pongezi kwa umoja wa wanafunzi waliowahi kusoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania – CAAT) kwa kuweza kuandaa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto), Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam.
Katika salamu zake Jaji Mihayo aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii ili waweze kujifunza mengi zaidi.
Burudani ya ngoma ikiendelea.
Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke akiingia ukumbini.
Vijana wakiwa katika picha ya pamoja.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni