.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 21 Desemba 2017

ANTU MANDOZA KUTIMIZA NDOTO YAKE YA KUIGIZA NA RAMSEY NOAH KUTOKA NCHINI NIGERIA

Antu Mandoza akiwa katika picha ya pamoja na Muigizaji nyota wa Filamu
kutoka nchini Nigeria Ramsey Noah wakiwa katika picha ya pamoja.

Mwigizaji nyota wa filamu na Mkongwe wa tasnia hiyo kutoka nchini Nigeria ,Ramsey Noah ametamani kufanya kazi na nyota mwingine wa movie anaechipukia kwa kasi katika tasnia hiyo hapa nchini, ambae ameng'ara vilivyo katika  filamu ya 'KIUMENI' , Antu Mandoza wa Tanzania .

"Anaonekana ni binti mweye kipaji,anaejiamini,kwa hakika natamani nipate muda wa  kubaini kipaji chake zaidi kwa kufanya nae angalau hata filamu
moja, itaweza kumsaidia zaidi kujitanua na kutambulika Kimataifa",alisema
Ramsey huku akimtazama Antu kwa tabasamu laini la ucheshi.

Antu Mandoza ni Binti wa makamo hivi, lakini amejaaliwa kuwa na kipaji cha
uigiza wa filamu na mwenye uthubutu wa kufanya jambo. Antu Mandoza na Ramsey Noah walikutana katika Warsha fupi iliyoandaliwa na Sahara Group
iliyofanyika hotel ya Hyatt Dar Es Salaam mnamo Desemba 16 2016, ambayo
pia iliwahusisha wasanii mbali mbali wa bongo movie .

Ikiwa ni movie yake ya kwanza 'KIUMENI', Antu Mandoza amefunguka na kusema  kuwa mwaka ujao utakua ni mwaka wa kazi tu, kama ilivyo Slogan ya Raisi  Dkt John Pombe Magufuli na anategemea kufanya kazi na Ramsey Noah na  wasanii wengine wengi wa Ndani na Nje ya Tanzania.


Antu alijipatia Umaarufu katika filamu ya Kiumeni aliyocheza na Ernest Napoleon, ambayo lishinda tuzo 2 ZIFF mwaka 2017.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni