.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 4 Desemba 2017

WAJASIRIAMALI JIJI LA ARUSHA WAPATIWA MKOPO WA MILIONI 605



Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akikabidhi hundi ya shilingi milioni 500 ya mkopo wa kinamama iliyotolewa na Halmashaur iya Jiji la Arusha. Na Woinde Shizza,Arusha

Jumla ya Shilingi milioni 605 zimetolewa kama mkopo wa kuwanufaisha wajasiriamali walioko kwenye vikundi vya kinamama na vijana pamoja na walemavu waliopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Akizungumzia mikopo hiyo inayotolewa na Halmashauri Afisa Ustawi wa Jamii Jiji la Arusha Hanifa Ramadhani amesema kuwa mikopo hiyo inatolewa ili kuwawezesha kinamama na vijana kuondokana na hali ngumu za kiuchumi zinazowakabili ili kuinua uchumi .

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro amewataka Vijana ambao ni wasomi kujiunga katika vikundi hivyo na kupata mikopo ili kujiendeleza kiuchumi badala ya kusubiri ajira serikalini ile hali nafasi ni chache na wahitimu wa vyuo ni wengi.

Kwa upande wao Wanufaika wa Mikopo hiyo kwaniaba ya Walemavu Mwajuma Juma na Patrick Petro wameishukuru serikali kwa kutoa mikopo hiyo yenye masharti nafuu ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni