Alexis Sanchez ameshuka ndimbani kwa
mara ya kwanza akiichezea Manchester United na kutoa pasi ya magoli
mawili kati ya manne yaliyopatikana dhidi ya Yeovil kwenye mchezo wa
kombe la FA mzunguko wa nne.
Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa
Chile, aliyejiunga na Manchester United akitokea Arsenal kwa
kubadilishana na Henrikh Mkhitaryan jumatatu, alianza kwa kucheza
pembeni kushoto katika dimba la Huish Park.
Sanchez alihusika mara kwa mara na
pasi za Manchester United jana usiku na pasi yake iliyomkuta Marcus
Rashford ilizaa goli katika kipindi cha kwanza na nyingine kwa Ander
Herrera nayo ikazaa goli la pili kipindi cha pili.
Katika mchezo huo Jesse Lingard
alifunga goli la tatu kabla ya Romelu Lukaku kufunga goli la nne
katika dakika ya mwisho, na kumzawadia kocha wao Jose Mourinho mwenye
miaka 55 zawadi ya siku yake ya kuzaliwa.
Marcus Rashford akifunga goli la kwanza la Manchester United baada ya kupewa pande na Sanchez
Romelu Lukaku akishangilia baada ya kufunga goli la nne katika dakika za mwisho wa mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni