.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 19 Machi 2018

WAZAZI WALEENI WATOTO WENU KATIKA MAADILI NA TAMADUNI ZA KITANZANIA

Naibu Katibu Mkuu Wazazi ccm Tanzania bara Godfrey Mheluka akiwa anawahutumia wananchi waliouthuria katika kongamano la kujadili maadili mema na uzalendo ni ustawi wa Arusha yetu na Taifa letu kwa ujumla ,kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Arusha ,kongamano ambalo lilishirikisha wananchi ,viongozi wa dini ,vyombo vya usalama pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wa sekta binafsi iliyofanyikia katika ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha
Kamanda wa vijana UVCCM mkoa wa Arusha Philemon Molel maarufu kama Monabani akiongea na wananchi waliouthuria katika kongamano la kujadili maadili mema na uzalendo ni ustawi wa Arusha yetu na Taifa letu kwa ujumla ,kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Arusha ,kongamano ambalo lilishirikisha wananchi ,viongozi wa dini ,vyombo vya usalama pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wa sekta binafsi iliyofanyikia katika ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha
                                                               
                                                             Habari picha na Woinde Shizza,Arusha

Wazazi wametakiwa kutimiza wajibu wao wa kuwalea watoto kwakufuata
maadili ya Mtanzania na kuacha kuiga tamaduni za kigeni ,kwani baadhi ya tamaduni za kigeni wanazo ziiga zinachangia kusababisha mporomoko wa maadili katika jamii zetu .

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wazazi ccm Tanzania bara
Godfrey Mheluka wakati akifunga kongomano la kujadili maadili mema
na uzalendo ni ustawi wa Arusha yetu na Taifa letu kwa ujumla ,kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Arusha ,kongamano ambalo lilishirikisha wananchi ,viongozi wa dini ,vyombo vya usalama pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wa sekta binafsi iliyofanyikia katika ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha

Alisema kuwa wazazi wengi wa wamekuwa wanalea watoto kwa kufuata
tamaduni za wenzetu wan chi za nje wakidai kuwa ndio malezi bora kwa
watoto na yakisasa kitu ambacho sio kizuri kwani baadhi ya tamaduni za
wenzetu ukiangalia za kutoka nchi za kimagharibi zinaporomosho maadili kwa watoto wetu.

“ukithamini tamaduni za kimagharibi na ukaacha za kwetu na ukamuacha
mtoto nae akathamini tamaduni hizohizo ujue umempoteza mtoto na
umemuaribu kabisa unakuta mzazi anaona mtoto anavaa mlegezo au kimini
badala ya kumkataza anamuacha anaona kuwa wake ndio mjanja huo sio
ujanja ni ujinga ni kumuaribu mtoto unatakiwa umwambie mtoto hivi sio vyema ivi nikiwauliza wazazi ivi nyie mngelelewa hivyo au mngelelewa vibaya je leo mngekuwepo apo mlipo ni wajibu wetu kuwalea watoto wetu kwa kufuata utamaduni wetu mzuri wenye maadili ili kuweza kuandaa viongozi wazuri wa baada na wazazi wazuri wa baadae “alisema Mhekuka

Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ccm mkoa wa Arusha
Dr,John Palanjo alisema ni wazazi anatakiwa kutimiza waji wake kwa mtoto wake huku pia mtoto akitakiwa kutimiza wajibu wake kwa mzazi ,aliongeza kuwa pia niwajibu wa kila mzazi kumfatilia mtotowake na kujua maendeleo yake mwenyewe na sio kumuachia mwalimu amfatilie au dada wa kazi amfatilie huku akibainisha kuwa mzazi yeyote asitafute mchawi wa mtoto wake kwani ,asilimia kubwa ya wazazi wao wenyewe ndio
wachawi wawatoto wao.

Aidha aliwaasa wazazi kutenga mda wa kukaa na watoto wao na kuongea na
kuwaelezea kipi kibaya na kipi kizuri ili kuwawezesha watoto wetu kukuwa kwa kuendana na yale yanayopendeza kwa jamii inayowazunguka

“mimi na imaini iwapo mzazi akijua wajibu wake atakubali hata kidogo mtoto wake aharibike ,hivyo ni vizuri mzazi utambue wajibu wako umrudie mungu usali maana ukiwa na hofu ya mungu lazima utamlea mtoto kwa kufuata kanuni za kimungu”alisema katibu wa wawazazi wilaya ya Arusha Christoper Pallangyo

Kwa upande wake mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Arusha Ally Meku aliwataka baadhi ya wazazi kupunguza migogoro ndani ya familia ili watoto nao wasiige tabia mbaya kwani wanapoaanza migogo katika familia wanashindwa kuwale watoto wao na badala yake watoto hao wanaanza kutangatanga hovyo na kuanza kuiga tabia mbaya.

                                           Baadhi ya viongozi wakiwa wanaimba na kucheza


                            Baadhi ya viongozi wakiwa meza kuu wanafatilia kongamano
RTO wa mkoa wa Arusha Josephy Bukombe nae alikuwepo katika kongamano hilo ambapo aliwasisitiza wazazi na vijana waliouthuria katika kongamano hilo kufuata maadili ,huku akiwasihi wazazi kuwakumbusha vijana wao kuvaa kofia ngumu wakati wanapoendesha pikipiki zao pamoja na kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kutokea mara kwa mara
Mkuu wa wilaya ya Arusha akiongea na wananchi waliouthuria katika kongamano hilo
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Edmond Rice nao waliuthuria katika kongamano hilo


Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ccm mkoa wa Arusha Dr,John Palanjo akiongea na wananchi waliouthuria katika kongamano hilo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni