Timu ya Liverpool imetinga nusu
fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu kupita
miaka 10 baada ya kutokea nyuma kufungwa goli moja na kuibuka na
ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Manchester City.
Wenyeji Manchester City walianza
vizuri kwa kumiliki mpira tangu mwanzo wakijaribu kubadili matokeo ya
mchezo uliopita ya kufungwa magoli 3-0 na alikuwa Gabriel Jesus
aliyefunga goli la kwanza.
Liverpool ilichomoa goli hilo katika
kipindi cha pili kupitia kwa Mohamed Salah mnamo dakika ya 56,
kufuatia pasi ya kutanguliziwa na Sadio Mane kisha baadaye zikiwa
zimesalia dakika 13 Roberto Firmino akaongeza la pili.
Mohamed Salah akifunga goli la kusawazisha lililochangia kubadilisha mchezo
Kocha Jurgen Klopp akipiga ngumi hewa kushangilia goli alilofunga Mohamed Salah
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni