TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tunapenda kuwaarifu kuwa leo hii tarehe 5 April 2018 Shirika la Posta (TPC) litatiliana saini mkataba wa kutoa huduma za usafirishaji barua na nyaraka muhimu kati yake na Mahakama ya Tanzania .
Mkataba huo utashuhudiwa na kusainiwa na Postamasta Mkuu na mtendaji Mkuu wa Mahakama ambaye ameongozana na Maofisa Waandamizi. Katika Ofisi za Mahakama ya Rufani zilizoko Jijini Dar es salaam.
Mkataba huu chini ya huduma mpya ya Posta mlangoni(The post at your doorstep) iliyoanzishwa na Shirika la Posta hivi karibuni ,utalipa jukumu la kukusanya na kusafirisha barua zote na nyaraka mbalimbali za mahakama na kuzifikisha kwa wahusika kulingana na anwani zao na mahali walipo (Anwani za makazi).
Kusainiwa kwa mkataba huu kutawezesha kuongeza kasi ya barua za kawaida, ya Mahakama kuwafikia walengwa mapema zaidi kwani zitakuwa zinachukuliwa Mahakamani na maofisa wa Posta na kupelekwa moja kwa moja kwa wahusika/ muhusika.
Shirika la Posta litatumia uzoefu wake wa muda mrefu kufanikisha jukumu hili, na hivyo kuzirahisishia mahakama zetu utendaji kwa kuwapunguzia mzigo wa ukusanyaji na usambazaji wa nyaraka zake hapa nchini.
Wito kwa Wananchi, tunawaomba watoe ushirikiano kwa maofisa wa Posta hususani kuandika anwani za makazi pamoja na postikodi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni