.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 10 Aprili 2018

NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUCHEZWA APRILI 20 NA 21

Hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam(ASFC) inatarajia kuchezwa Aprili 20 na Aprili 21,2018.

Nusu fainali ya Kwanza itachezwa Ijumaa Aprili 20,2018 ikiwakutanisha Stand United ya Shinyanga watakaokuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Kambarage,Shinyanga saa 10 jioni.

Singida United ya Singida watawakaribisha JKT Tanzania ya Dar es Salaam kwenye nusu fainali ya pili itakayochezwa Uwanja wa namfua Jumamosi Aprili 21,2018 saa 10 jioni.

Washindi kwenye nusu fainali hizo watacheza mchezo wa fainali May 31,2018.

LIGI KUU YA WANAWAKE YA SERENGETI PREMIUM LITE NANE BORA KUENDELEA APRILI 21

Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite hatua ya Nane bora inatarajia kuendelea Jumapili Aprili 21 kwenye viwanja tofauti.

Hatua hiyo ya nane bora ambayo ilisimama kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Wanawake(Twiga Stars) iliyokuwa kambini kujiandaa na mchezo wake wa kufuzu fainali za Africa kwa Wanawake itaendelea katika mzunguko wa Tano(5).

Hatua ya nane bora inachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ikishirikisha timu za Panama FC ya Iringa inayotumia Uwanja wa Samora, Evergreen Queens ya Dar es Salaam inayotumia Uwanja wa Karume, JKT Queens ya Dar es Salaam wanaotumia Uwanja wa Mbweni, Alliance ya Mwanza wanaotumia Uwanja wa Nyamagana, Mabingwa watetezi Mlandizi Queens ya Pwani wanaotumia Uwanja wa Mabatini, Baobab ya Dodoma wanaotumia Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Kigoma Sisters ya Kigoma wanaotumia Uwanja wa Lake Tanganyika na Simba Queens wanaotumia Uwanja wa Karume.

Huu ni msimu wa pili wa Ligi ya Wanawake kuchezwa ambapo katika msimu wake wa kwanza timu ya Mlandizi Queens ndio waliibuka na ubingwa.

Ligi hiyo inadhaminiwa na Bia ya Serengeti Premium Lite yenye ladha maridadi.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni