Na Richard Mwaikenda, Kivule, Dar.
Viongozi wa Kata ya Kivule, Ukonga Dar, wameunganisha nguvu kuwasaka vipaka wanaowapora watu wanaopita wakati wa usiku katika Daraja linalojengwa katika MTO Kizinga.
Uamuzi huo umefanywa baada hivi karibuni Majira ya SAA 5 usiku ambapo mtu mmoja aliyekuwa akivuka katika Daraja la muda kuporwa na vibaka Simu na vitu vingine.
Tukio hili aliliripoti kituo kidogo cha POLISI cha Kitunda, na kwa viongozi wa Kata ya Kivule, akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kivule, Amos Angaya na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kerezange, Ismail Ibrahim.
Mwandishi wa Habari hii alishuhudia viongozi hao wakiwa wamemuweka chini ya ulinzi, Kijana Jaffari aliyekamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika uporaji huo akishirikiana na wenzie.
Viongozi hao walimnasa 'Kibaka' huyo kwa ushirikiano Mkubwa na waendesha bodaboda pamoja na wafanyabiashara ndogondogo wanaoendesha shughuli zao darajani hapo.
Walimnasa Jaffari baada ya kutumia mbinu ya kuwatishia wanaoendesha shughuli zao darajani hapo kwamba wasipowataja vibaka basi wote watafukuzwa eneo hilo.
Walimnasa Jaffari baada ya kutumia mbinu ya kuwatishia wanaoendesha shughuli zao darajani hapo kwamba wasipowataja vibaka basi wote watafukuzwa eneo hilo.
Kwa umoja wao, viongozi hao waliapa kutokomeza vitendo vya uovu vilivyoanza kuota mizizi katika eneo hilo la Daraja ambalo limekata mawasiliano ya usafiri Kati ya Kivule Mwembeni na Silari baada Daraja bovu kuvunjwa na kuanza kujenga jipya.
Kwa.mujibu wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kerezange, Ismail Ibrahim, Ujenzi wa Daraja hilo unatarajiwa kukamilika Mei, Mwaka huu.Hivi sasa daladala kutoka Banana zinaishia upande wa Mwembeni na zinazotoka Frem kumi zinaishia Silari. Magari mengine yanapitia Daraja la Bombambili.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni