.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 16 Aprili 2018

WAZIRI MHAGAMA AKAGUA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MEI MOSI - IRINGA

                                                                                    Na.MWANDISHI WETU

Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amekagua maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi na kusema ameridhishwa na hatua zilizofikiwa.

Ametoa kauli hiyo Aprili 14, 2018 baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya Maandalizi katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Waziri amesema Kamati ya Mkoa imefanya vizuri hatua iliyomfanya kuridhishwa na maandalizi hayo.

“Nitoe pongezi kwa hatua hizi za awali mlizoanza nazo ikiwemo Kuunda kamati hii ya kuratibu shughuli zote ili kuhakikisha sherehe hizi zinafana na kuvunja rekodi.”Alisema waziri.

Waziri aliwataka wanakamati hao wahakikishe wanasimamia vizuri wageni, pamoja na wananchi watakaojitokeza kwa kuzingatia jiografia ya Viwanja vya Samora.

“Niwaombe mzingatie namna bora ya kuwaratibu wageni watakaohudhuria, na kuangalia namna ya kuwapanga wananchi kwa kuzingatia uwanja huu umezungukwa na wakazi wengi hivyo tunatarajia ugeni mkubwa.”Alisisitiza Waziri.

Sambamba na aliwaomba waendelee kuhabarisha umma ili Wananchi wafike kwa wingi ikiwemo Wajasiliamali wadogo ili kupata fursa ya kujitangaza na kuonesha namna mkoa unavyozalisha na kuchangia katika uchumi wa viwanda.

Aidha kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza aliahidi kusimamia vyema maandalizi na shughuli zote kwa ufanisi na kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa.

“Ninaahidi kusimamia vyema yote uliyoelekeza na kutekeleza kwa ufanisi, na tunakupongeza kwa kutembelea kuangalia namna tunavyoendelea na maandalizi, nikuhakikishie tumejipanga kama Askari vitani, wakati wote tu tayari.”Alisisitiza Mhe. Masenza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisalimiana na baadhi ya wanakamati wa Maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi zitakazofanyika Kitaifa mkoani Iringa alipotembelea kukagua maandalizi yanavyoendelea Aprili 14, 2018.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiweka saini katika kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza ili kukagua maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza akitoa maelezo mafupi kuhusu maandalizi ya sherehe za Mei Mosi kwa Mhe Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu alipotembelea katika Ofisi zake Iringa.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa kikao kifupi na baadhi ya Wanakamati ya Maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi mkoani Iringa.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi wakifuatilia maagizo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipotembelea kukagua Maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza akiwasilisha taarifa ya Maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi wakati wa kikao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama.
 Katibu wa Kamati ya Itifaki Bw. Fuad Mwasiposya akitoa maelekezo kuhusu Uwanja wa Samora kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa maandalizi hayo Mkoani Iringa.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza katika Viwanja vya Samora Iringa.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akitoa maelekezo kuhusu ukumbi wa Kichangani utakao tumika wakati wa Kongamano la Maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi litakalofanyika tarehe 27 Aprili, 2018 Mkoani Iringa.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akitoa maelekezo kwa Kamati ya Maandalizi ya Mei Mosi kuhusu mpangilio wa Uwanja wa Samora utakaotumika siku ya Maadhimisho hayo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi Mkoani Iringa.

                                                                 (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni