Ijumaa, 13 Aprili 2018
WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI KUMBUKUMBU YA MIAKA 34 YA KIFO CHA EDWARD SOKOINE
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mjane (mke mkubwa) wa marehemu Edward M. Sokoine Bibi Napono Sokoine, mara baada ya kuwasili nyumbani kwao kushiriki ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika leo Aprili 12, 2018. Kulia ni mke mdogo, Bibi Nekiteto Sokoine. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mjane (mke mkubwa) wa marehemu Edward M. Sokoine Bibi Napono Sokoine, akimvisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mgolole wa Kimasai ikiwa ni ishara ya kumkaribisha nyumbani kwao, kijiji cha Engwiki, kata ya Monduli Juu, wilayani Monduli, mkoani Arusha leo Aprili 12, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo ya marehemu Edward M. Sokoine kabla ya kuanza kwa ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika leo Aprili 12, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwaongoza viongozi wa mkoa wa Arusha na wa Serikali kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika leo Aprili 12, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasalimia wanafamilia baada ya kutoa salaam zake kwa wananchi waliohudhuria ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika leo Aprili 12, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiomba dua baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Sokoine mara baada ya kuhudhuria ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika leo Aprili 12, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni