Hii sikukuu
imekuja vizuri lakini kwa wengine imewajia vibaya kabisa.
Huyu mzee
akiwa chakari kwa kinywaji, yaani kalewa sawasawa, jana alipita karibu na eneo
la kutupa takataka lililopo kwenye bar fulani maeneo ya Mikocheni.
Alipokuwa
katika eneo lile la taka, akaona chupa mbalimbali za bia zikiwa zimetupwa eneo
lile. Basi akaokota chupa tupu ya kwanza kisha akaibamiza ukutani huku akisema “
kwasababu yako nimeachana na mke wangu”
Akaokota
tena chupa tupu ya pili nayo akaibamiza ukutani huku anasema “ kwasababu yako
nimeshindwa kuwasomesha watoto wangu”
Akaokota
chupa tupu ya tatu nayo akaibamiza ukutani huku akisema “ kwasababu yako
umesababisha nikauza nyumba yangu”
Alipookota
chupa ya nne, ile kuinyanyua juu akakuta ndani ina bia, yaani haijafunguliwa
kama zile nyingine alizozivunja, basi akaitazama weee kisha akasema:-
“ We sina
ugomvi na wewe kabisa, basi akaifungua na kuanza kunywa huku akisema, wewe huna
mabaya kama hawa wenzako , wewe ni rafiki wa kweli na nakupenda sana”
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni