.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 13 Oktoba 2013

MWANDISHI WA HABARI WA ITV/RADIO ONE AMEPIGWA RISASI NA KUJERUHIWA VIBAYA, MAMA YAKE AUAWA

Mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Bwana Anthery Mushi, amempiga risasi Mwandishi wa Habari wa ITV/Radio One , Ufoo Saro na kumjeruhi vibaya.

Aidha Anthery Mushi amempiga risasi  kumuua mama yake mzazi  Ufoo Saro na kisha kujiua, katika tukio lililotokea leo asubuhi maeneo ya Kibamba CCM, Wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam.


Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Kinondoni, Bwana  Camilius Wambura  amesema tukio hilo limetokea saa 12 na nusu leo asubuhi na kusema inadaiwa kuwa Anthery Mushi ni mume au mchumba wa Ufoo Saro  anafanya kazi Umoja wa Mataifa na kituo chake cha kazi ni nchini Sudan.


Kamanda WAMBURA amesema Anthery Mushi  alirejea jana kutoka Sudan na leo majira ya saa 12 waliondoka yeye  na Ufoo Saro  wakitokea eneo la Magari Saba kwenda kwa Mamake  Ufoo Saro, Kibamba CCM.


Amesema kilichoendelea huko bado askari wanaendelea na uchunguzi, lakini taarifa zinasema walipofika huko Anthery Mushi alichukua bastola na kumpiga risasi  kifuani mama mzazi wa Ufoo Saro na  na kisha kumpiga Ufoo risasi  tumboni na mguuni  kisha yeye kujipiga risasi juu ya kidevu na kufariki dunia papo hapo.


Ufoo Saro alikimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako anapatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dakta Reginald Mengi, amefika katika hosptiali hiyo kumjuilia hali  Ufoo Saro.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni