Hizi ndoa
ngumu sana, ukiona watu wamedumu katika ndoa miaka 20 ujue wamepitia mapito
mengi, lakini kikubwa wamevumiliana sana.
Mzee mmoja ambaye kila siku alikuwa haishi kugombana na mkewe, jana akiwa Brake Point Kijitonyama anapata kinywaji huku akionekana kuna jambo linamsumbua sana kichwani.
Akiwa katika hali ile ya mawazo, akachukua simu yake na mkononi na kumtumia ujumbe mfupi ( sms ) mkewe aliyekuwa nyumbani kwa muda ule.
“Vipi wife habari za saa hizi?'.
Baada ya dk 5 mkewe akamjibu:-
“Nafa Mume wangu nafa”.
Alipousoma ule ujumbe wa mke wake, mara mume akashuka kwenye kiti cha bar na kuanza kucheza kiduku kwa furaha kubwa, kisha akaagiza mzinga mzima wa konyagi, na kutoa ofa kwa jamaa waliokuwa pembeni yake ambao hata hawajui.
Akiwa katika hali ile ya furaha huku wateja wengine pale bar wakimshangaa, mara ukaingia ujumbe mfupi kwenye simu yake.
Alipoufungua asome,akakuta umetoka kwa mkewe na unasomeka hivi:-
'Samahani mume wangu nimekutumia sms naona imekatika inasomeka NAFA, nilikuwa namaanisha “NAFANYA USAFI HUKU JIKONI”
Mzee akaanguka chini akapoteza fahamu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni