.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 12 Oktoba 2013

KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE KUKUTANA DAR KUANZIA JUMANNE TAREHE 15 HADI 26 OKTOBA, 2012

images (2) 
Kwa kawaida, wiki mbili kabla ya Mkutano wa Bunge, Kamati za Kudumu za Bunge hukutana ama Dar es Salaam, Dodoma au Zanzibar kwa mujibu wa Kanuni ya 114(3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007. 

 Kuanzia tarehe 15 hadi 26 Oktoba 2012 Kamati hizo zitakutana Jijini Dar es Salaam kabla ya Mkutano wa Tisa wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 30 Oktoba hadi 09 Novemba, 2012. Hata hivyo Kamati ya Nishati na Madini haitakuwepo kutokana na kuvunjwa wakati wa Mkutano wa Nane wa Bunge la Kumi.

Aidha Wabunge wote wanapaswa kuwa wamewasili jijini Dar es Salaam ifikapo jumapili tarehe 14 Oktoba 2012 tayari kwa kuanza vikao siku inayofuata.
 

SHUGHULI ZITAKAZOTEKELEZWA
 

Shughuli za jumla:
 

Uchambuzi wa Muswada mmoja wa Sheria Kushughulikia maazimio manne ya Bunge
Kupokea Taarifa mbalimbali kutoka Wizara na Taasisi za Umma na Binafsi
Ziara fupi Jijini Dar es Salaam
Ziara ndefu nje ya Dar es Salaam
Kupitia Hesabu zilizokaguliwa 2010/2011
Hesabu za Mashirika ya Umma
Hesabu za Serikali za Mitaa
Hesabu za Serikali Kuu
Maazimio ya Bunge

Kamati tatu zitakuwa na kazi ya kushughulikia maazimio manne ya Bunge kuridhia Mikataba mitatu na Itifaki moja. Kamati hizo ni:-
Kamati ya Fedha na Uchumi – Azimio moja la Mkataba
Kamati ya Miundombinu –Azimio moja la Mkataba na moja la Itifaki
Kamati ya Huduma za Jamii – Azimio moja la Mkataba
Taarifa za Utendaji

Kamati kumi zitapokea na kujadili Taarifa za Utendaji wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa majukumuya Serikali kupitia Wizara na Taasisi hizo.
ZIARA

Kamati tisa zitafanya ziara fupi na ndefu kwa madhumuni ya kufuatilia utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Serikali na Taasisi zake.

Imetolewa na: Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,

Ofisi ya Bunge

Dar es Salaam

13 Oktoba 2012

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni