Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Afrika
wanakutana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kujadili uhusiano wa bara
la Afrika na mahakama ya kimataifa ya jinai ICC.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ethiopia Tedros Adhanom Ghebreyesus, ameilaani mahakama ya ICC kwa kusema ina mapendeleo sana, na hicho sio kitu kinachokubalika, kwani inaoneka inazikandamiza nchi za Afrika.
Waziri huyo ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao maalum cha AU kuhusu mahakama ya ICC.
Kikao hicho kinafuatia ombi la serikali ya kenya.
Umoja wa Afrika unaishtumu mahakama ya ICC kwa kuwalenga viongozi wa bara hilo, huku ikipuuzilia mbali uhalifu mwengine dhidi ya binadamu unaotekelezwa katika maeneo mengine ulimwenguni.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho waziri wa maswala ya kigeni kutoka Ethiopia Tedros Adhanom ameishtumu mahakama hiyo kwa kukataa kuheshimu uwezo wa Marais wa bara la Afrika, na kukitaka kikao hicho kushutumu mahakama hiyo.
Mkutano huu maalum umeitishwa baada ya ICC kukataa ombi la wanachama 34 wa Muungano wa Afrika kurejesha kesi za Rais wa Kenya Mh Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto nyumbani.
Miongoni mwa yatakayozungumziwa ni hoja ya kujiondoa kutoka katika mahakama hiyo.
Baada ya miezi kadhaa ya kutofautiana kati ya ICC na AU, viongozi wa Afrika wanakutana katika makao makuu ya AU katika kile kinachosemekana ni kutafakari upya uhusiano wa bara hilo na mahakama ya ICC.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni