.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 14 Desemba 2013

KWAHERI NELSON MANDELA, KUZIKWA KESHO KIJIJINI QUNU

            Mwili wa Nelson Mandela ukiondolewa katika majengo ya Umoja
     Picha za maandalizi ya mwisho mwisho kijijini Qunu kabla ya maziko kesho


Jeneza la Mandela jana liliondolewa kutoka katika jumba la umoja ( Union Buildings ) baada ya shughuli za kutoa heshima za mwisho kumalizika huku maelfu ya waombolezaji wengine wakikosa nafasi hiyo baada ya kusitishwa rasmi

Hata hivyo mwili wa Mandela ulisalia mjini Pretoria ambapo  usiku kucha wa kuamkia leo jumamosi kulikuwa na hafla maalum ya viongozi wa ANC nao kutoa heshima zao za mwisho kwa Mandela katika mojawapo ya kambi za jeshi.

Jeneza la Mandela hata hivyo lipatapelekwa kwa ndege nyumbani kwao katika kijiji cha Qunu mkoa wa Western Cape tayari kwa mazishi ambayo yatafanyika kesho jumapili.

Mazishi ya Mandela yatakuwa kikomo cha maombolezi ambayo yamefanyika kwa siku kumi tangu afariki dunia alhamisi iliyopita ya tarehe 5 Disemba.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni