Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir,amesema kuwa jeshi limetibua njama za mapinduzi dhidi ya serikali yake.
Rais Kiir amewalaumu wanajeshi wanaomuunga mkono aliyekuwa naibu wake Riek Machar ambaye alifukuzwa kazi, kwa mapigano yaliyozuka kati ya wanajeshi wake Jumapili usiku.
Akiongea na waandishi wa habari, Bwana Kiir alisema serikali imedhibiti hali huku ikitangaza sheria ya kutotoka nje nyakati za usiku.
Wanajeshi mahasimu, walipigana vikali kwa masaa kadhaa na inaarifiwa kuna majeruhi kadhaa huku mamia wakitoroka mji wa Juba.
Kwa sasa milio ya risasi imekwisha. Kumekuwa na hali ya taharuki nchini Sudan Kusini tangu mwezi Julai wakati Rais Kiir alipowafukuza kazi mawaziri wake akiwemo bwana Machar.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni