Rais Barack Obama wa Marekani ameahidi
kutopitisha kwenye baraza la Congress baadhi ya maamuzi yake ya
kukabiliana na tofauti za hali ya kiuchumi nchini mwake, katika
hotuba yake aliyoitoa kwa taifa.
Katika hotuba yake hiyo ya kwanza kwa
taifa la Marekani kwa mwaka huu, Rais Obama ameahidi kuchukua hatua
bila kupitia chombo hicho pale inapobidi, na kutangaza nyongeza ya
mishara kwa watumishi wapya wa serikali walio kwenye mikataba.
Rais Obama pia amesisitiza juu ya
kuwawezesha wanawake ambapo amesema wanawake wanatoa mchango mkubwa
kwa taifa la Marekani na iwapo watafanikiwa kiuchumi na taifa hilo
pia litafanikiwa kiuchumi.
Pia amesisitiza kufungwa kwa gereza la Guantanamo na kumaliza kazi iliyowapeleka Afghanistan mwaka huu.
Rais Obama amegusia pia kurekebishwa kwa sheria ya kumiliki silaha kwa Wamerekani, sheria za uhamiaji, kudhibiti uchafuzi wa hewa pamoja na uzalishaji viwandani na kuongeza ajira.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni