Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Bw. Meck Sadick akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Mandela Road . Kwanza kushoto ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam , Bw. Salie Mlay na kwanza kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa wateja wakubwa NMB, Bw.Gerald Kamugisha wakishuhudia ufunguzi huu uliofanyika jana jijini Dar es salaam.
Menejawa NMB kanda ya Dar es salaam, Bw.Salie Mlay akimwelezea Mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam (kwanza kushoto, Bw. Meck Sadick huduma mbalimbali zitolewazo na tawi jipya la NMB mandela Road
Tawi hili litakua wazi kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni ( 2:30 asubuhi – 10:30 jioni) na Jumamosi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana (8:30 asubuhi- 6:30 jioni), Jumapili na siku za sikukuu hakutakuwa na huduma ndani ya tawi hili.
Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Bw. Meck Sadick (kwanza Kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vifaa vya hosipitali Mganga mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana ,Dr Meshack Shimwela .Mashuka ya Hospitali pamoja na Vitanda vya wodi ya akina mama ni miongoni mwa vifaa vilivyotolewa .Makabidhiano haya yamefanyika jana wakati wa uzinduzi wa tawi la NMB mandela Road Katikati ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam, Bw.Salie Mlay.
Katika kusherehekea ufunguzi rasmi wa tawi hili, Benki ya NMB ilitoa msaada kwa jamii wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni kumi ili kuunga mkono jitihada za serikali na wananchi katika kuboresha huduma katika sekta ya afya. Msaada huu unatolewa kwa hospitali ya Amana pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Bw. Meck Sadick (wapili kulia kwenye viti) akiwa kwenye picha ya Pamoja na maafisa wa NMB tawi la Mandela Road


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni