Jengo la ghorofa 17 ambalo linafanana
na mti linatarajiwa kujengwa huko Montpellier nchini Ufaransa,
kuanzia mwakani.
Jengo hilo la makazi litajulikana kama
“The White Tree” ama kwa lugha ya Kiswahili Mti Mweupe, litakuwa
na umbo mithili ya matawi yanayotoa kivuli na kuvuta mwanga kuingia
ndani yake.
Kazi ya usanifu wa jengo hilo imefanywa
na msanifu Mfaransa na Wajapani litakuwa na baa kwa juu, hoteli na
sehemu ya sanaa za michoro, huku watu wakipata kuona vyema mlima na
bahari.
Pia litakuwa na nyumba za makazi 120,
zenye vyumba na muondo wa aina tofauti kulingana na mahitaji ya
familia.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni