Zaidi ya magari 2,000 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4 za
Kenya yanatarajiwa kuharibiwa nchini humo kutokana na kutengenezwa
miaka 8 iliyopita, na kuingizwa kinyume na sheria za Kenya.
Tume ya Maadili na Rushwa imeagiza gari hizo zinazoshikiliwa katika
bandari ya Mombasa kupondwa pondwa kwa kuwa inachukulia suala la
rushwa katika mipaka ya Kenya kwa umakini mno.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Muno Matemu amesema uchunguzi unaendelea
kubaini ni kwa namna gani magari hayo yaliingia Kenya, licha ya
taifa hilo kupiga marufuku kuingizwa nchini magari yaliyopita miaka
nane tangu yatengenezwe.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni