.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 6 Machi 2014

MECHI ZA KIMATAIFA ZA KIRAFIKI, UINGEREZA YAICHAPA DENMARK, AFRIKA KUSINI YABAMIZWA NA BRAZIL 5-0, UJERUMANI NAYO YATAMBA

 Usiku wa leo kulikuwa michezo mingi tu ya kimataifa ya kirafiki iliyopo katika kalenda ya Fifa, ambapo katika michezo hiyo Ujerumamani imeifunga Chile bao 1-0, bao ambalo liliwekwa kimiani na Mario Gotze ( pichani juu ) baada ya kupokea pasi safi toka kwa Mesut Ozil
 Mesut Ozil akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Chile
 Kwinginenko Uingereza ilifanikiwa kuifunga Denmark bao 1-0, bao ambalo lilifungwa na Daniel Sturridge

 Yenyewe Poland iliifunga Scotland bao 1-0, bao ambalo lilifungwa na Scott Brown ( pichani juu )
                        Mashabiki wakifuatilia mchezo huo wa Poland na Scotland
 Mechi nyingine ilizikutanisha Ireland na Serbia, mchezo uliomalizika kwa Ireland kufungwa na Serbia mabao 2-1

 Mjini Soweto Afrika kusini ilikuwa na siku mbaya nyumbani kwao baada ya kukubali kipigo kikali cha mabao 5-0 toka kwa Brazil ambao ni wenyeji wa kombe la Dunia mwaka huu. Mabao ya Brazili yalifungwa na Neymar ambae alifunga mabao 3 katika mguu wake mwenyewe, huku Oscar na Fernandinho wakifunga bao moja moja
                         Furaha ya kuitandika Afrika Kusini 5-0
 Mshambuliaji wa Wales, Gareth Bale jana aliisadia nchi yake kuifunga Iceland mabao 3-1 katika mchezo mwingine wa kimataifa wa kirafiki

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni