.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 5 Machi 2014

MVUA KUBWA KUNYESHA KATIKA SAA 24 ZIJAZO



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa tahadhari kwamba mvua kubwa inayozidi milimita 50 inatarajiwa kunyesha ndani ya saa 24.

Maeneo yanayotarajiwa kupata mvua hizo ni ukanda wa Pwani yenye mikoa ya Mtwara, Lindi,Pwani, Dar es Salaam,Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Taarifa hiyo ya mamlaka ya hali ya hewa nchini imesema hali hiyo imetokana na kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa hewa Mashariki mwa Bahari ya Hindi pamoja na kusogea kwa haraka kwa mfumo wa mvua za msimu, hivyo kuongeza kiwango cha unyevunyevu kutoka baharini kuelekea maeneo yaliyotajwa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni