.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 10 Machi 2014

OSCAR PISTORIUS ATAPIKA KIZIMBANI WAKATI DAKTARI AKITOA USHAHIDI

Oscar Pistorius ametapika kizimbani hii leo wakati mtaalam aliyeufanyia uchunguzi mwili wa aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp akitoa maelezo ya kimichoro yanayoonyesha jinsi marehemu alivyoumia.

Mwanariadha huyo mlemavu alienda kwenye ndoo ya taka kutapika wakati Profesa Gert Saayman akitoa maelezo ya kutisha kuhusiana majeraha kadhaa ya risasi aliyomsababishia mpenzi wake siku ya tukio hilo.
Profesa Saayman ameiambia mahakama Miss Steenkamp alipigwa risasi mara nne katika eneo la juu la kulia la kichwani, kwenye kiwiko cha mkono wa kulia, kwenye paja la kulia na upande wa mkono wa kushoto.

Wakati ushahidi huo ukitolewa mahakama ililazimika kuhairisha mara mbili wakati Pistorius alipoangua kilio huku mabega yake yakitetemeka


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni