.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 14 Machi 2014

SAMUEL SITTA NA SAMIA SULUHU HASSAN WAPONGEZWA KWA KUCHAGULIWA KWAO KULIONGOZA BUNGE MAALUM LA KATIBA


Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Tanzania ambae pia ni Waziri wa Nchi anayeshughulikia Muungano Mh.Samia Suluhu Hassan Kushoto akiwa pamoja na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi katika Tafrija ndogo ya kuwapongeza Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo mara baada ya kuchanguliwa kuliongoza Bunge hilo linaloendelea kukutana Mjini Dodoma.

Washiriki wa Tafija fupi ya Kupongezwa kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh. John Samule Sita na Makamu wake Mh. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika katika Mkahawa wa China uliomo ndani ya Dodoma Hoteli.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mh. Moh’d Aboud Moh’d akifanya mzaha kunogesha tafrija ya kupongezwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Hapo Dodoma Hoteli.
Kulia ya Waziri Aboud ni Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar Mh. Salum Turky, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh. John Samuel Sita pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh. John Samuel Sita akitoa neno la shukrani mara baada ya Tafrija fupi ya kupongezwa kwake yeye na Makamu wake Mh. Samia Suluhu hapo Chinese Restaurant Mjini Dodoma.


Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akizungumza katika Tafrija fupi ya kupongezwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma.

Kushoto yake ni Mumewe Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na baadhi ya watendaji wa Ofisi yake.

                                         Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni