.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 9 Machi 2014

WATUMISHI WA UMMA NCHINI KENYA WAGOMA MISHAHARA YAO KUPUNGUZWA

Watumishi wa umma nchini Kenya wameapa kupinga uamuzi wa kupunguzwa kiwango cha mishahara yao ili kudhibiti mzigo mkubwa wa mishahara unaoielemea serikali, licha ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kuagiza nao mishahara yao ipunguzwe.

Rais Uhuru na Naibu wake Ruto waliafikiana kukubali kukatwa asilimia 20 ya mshahara yao, ambapo pia mawaziri wa serikali ya Kenya nao walikubali kupunguzwa asilimia 10 ya mshahara wao katika kudhibiti mzigo wa mishahara ya umma unaozidi kuongezeka.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni