Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shaabani Hassan,wakati wa uhai wake.
Baadhi ya wanafamilia wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shaabani Hassan wakiteremka katika ndege ya Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ,baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,ikiwa na mwili wa Marehemu huyo.
Ndugu na Jamaa wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shaabani Hassan,wakilia kwa uchungu baada ya kufika mwili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,tayari kwa mazishi yake yatakayofanyika leo kwa heshima zote za Kijeshi katika makaburi ya Tomondo Wilaya magharibi Unguja.
Wanajeshi wa JWTZ hapa Zanzibar wakiuteremsha mwili wa marehemu Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shaabani Hassan,kutoka katika Ndege ya jeshi hilo iliyotua leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ukitokea katika Hospitali ya Jeshi Lugalo baada ya kufariki juzi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni