Machi 4, 2014; Kampuni ya Bia ya Serengeti inatarajia
kuchezesha droo ya nne ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti
ambapo mshindi wa kwanza wa kwenda Brazili atapatikana. Licha ya zawadi kibao
kutoka kampuni hiyo kama ving’amuzi, ipad, bia za bure, na fedha taslimu
kufaidisha wateja wengi wa bia ya Serengeti kwa wiki tatu za mwanzo na
zinazoendelea, wiki hii kutakua na zawadi kubwa zaidi ya promosheni hiyo ya
safari ya kwenda Brazili ambapo mshindi atalipiwa gharama zote kwenda kutembea
nchini humo.
Wakiongea kwa nyakati tofauti washindi wa wiki ya tatu ya
promosheni hiyo wameonesha furaha zao kwa kupata zawadi hizo huku wakiishukuru
Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwajali wateja wake huku wengi wao wakiwa na
shauku ya kupata zawadi kubwa zaidi ya promosheni hiyo ya kwenda nchini Brazil
ambayo droo yake itachezeshwa wiki hii huku gharama zote zikilipwa na Kampuni
ya Bia ya Serengeti.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika
mapema wiki hii mmoja wa washindi wa Samsung tablet Vedastus Kalinga kutoka
Mbeya alisema amefarijika sana kupata zawadi ya simu hiyo ya mkononi kutoka
Kampuni ya Bia ya Serengeti kwani itamsaidia kufanya vitu vyake kwa urahisi
zaidi katika ulimwengu huu wa dijitali ingawa ndoto yake ni kupata safari ya
kwenda Brazili.
Naye Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo alisema mpaka
sasa washindi watano wameshakabidhiwa simu aina ya ‘Samsung Galaxy tab 3’ na
kumi na nne wameshapata ving’amuzi kupitia promosheni ya Winda Safari ya
Brazili na Serengeti. Promosheni hiyo zaidi ya zawadi za washindi wa droo za kila
wiki pia kuna washindi wa bia za bure za papo hapo na fedha taslimu ambapo
zaidi ya wateja 716 wameshajipatia fedha
taslimu Tsh 5000 na washindi 400 wameweza kujipatia Tsh 10,000 .
“Tunapenda kuwataarifu wateja wetu kuwa wiki hii kutakuwa na
droo kubwa yakupata mshindi wa kwanza wa safari ya Brazili ambaye atalipiwa
gharama zote na Kampuni ya Bia ya Serengeti. Zawadi hii kubwa ni kwaajili ya wateja
wetu chakufanya ni kufungua bia yako ya Serengeti kokote nchini na fuatilia
maelezo ya promosheni na uweza kuwa mshindi wetu wa wiki inayokuja. Pia unaweza
kufuatilia kupitia ukurasa wetu wa facebook
www.facebook.com/serengetipremiumlager. Hivyo hatuna budi kuwashukuru wateja
wetu kwa ushirikiano wanaotupa”, aliongeza Rugambo.
Kunywa
kwa tahadhari. Inauzwa kwa wenye miaka 18+.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni