Mamia ya boti, helkopta za uokoaji na wazamiaji wameendelea na harakati za uokoaji wa mamia ya abiria waliokuwa katika kivuko kilichokuwa na abiria 470 kilichozama huko Korea Kusini.
Tayari watu 164 wameokolewa huku taarifa zikisema watu 4 wamefariki dunia katika ajali hiyo.
Kati ya waliofariki ni pamoja mwanamke mwenye miaka 27 aliyetambulika kwa jina la Park Ji-Yeong na mwanafunzi Jeong Cha Woong.
Mpaka sasa zaidi ya abiria 300 ambao wengi wao ni wanafunzi waliokuwa wanasafari na kivuko hicho bado hawajaokolewa na juhudi za kuwatafuta zinaendelea kwa kasi kubwa. Walikuwa wanaelekea katika kisiwa cha kusini cha Jeju
Sehemu ya kivuko hicho inavyoonekana wakati ikiendelea kuzama baharini
Mamia ya boti za uokoaji zikijumuisha za wavuvi zikielekea kilipo kivuko hicho tayari kutoa msaada wa waathirika
Mmoja wa walionusurika katika ajali hiyo akiokolewa kwa kutumia helkopta
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni