.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 16 Aprili 2014

ARSENAL YAZINDUKA LIGI KUU UINGEREZA, YAICHAPA WEST HAM 3-1

 Timu ya soka ya Arsenal imefufua matumaini ya kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao, baada ya usiku wa kuamkia leo kuichapa West Ham mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliochezwa katika uwanja wa Emirate.
 Katika mchezo huo, mabao ya washika bunduki hao yaliwekwa kimiani na Podolski ambaye aliifungia timu yake mabao mawili kunako dakika ya 44 na 78 na bao jingine likifungwa na Giroud dakika ya 54. Bao la West Ham liliwekwa kimiani na Jarvis kunako dakika ya 40
Kwa matokeo hayo Arsenal ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 67. Nafasi ya kwanza wamesimama Liverpool wenye point 77, nafasi ya pili wapo Chelsea wenye pointi 75 na Manchester City wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 70

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni