.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 24 Aprili 2014

GARI LINGINE LAKUTWA NA MLIPUKO KARIBU NA SHULE YA SEKONDARI YA DON BOSCO MJINI NAIROBI

Gari linalosadikiwa kuwa limebeba mlipuko limekutwa limetelekezwa nje ya uzio wa shule ya Sekondari ya Don Bosco katika mtaa wa Pangani, jijini Nairobi leo asubuhi. 

Iliwabidi polisi kutumia mbwa maalum ili kulikagua gari hilo. Wizara ya mambo ya ndani imethibitishwa kukutwa kwa mlipuko ndani ya gari hilo. 

Kenya imekuwa ikabiliwa na vitendo vya kigaidi kwa siku za karibuni, na jana watu 4 walifariki dunia baada ya kulipukiwa na bomu katika kituo cha Polisi cha Pangani, bomu hilo lililokuwa ndani ya gari lililokamatwa na polisi

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni