Gavana wa Shirika
la Lions Club nchini Bwana Wilson Ndesanjo akimvika Rais Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete medali maalum ya Uongozi Bora na mahusiano mema wakati
wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo
asubuhi.Bwana Ndesanjo alisema klabu hiyo imeamua kumtunuku Rais
Kikwete medali hiyo kwa kutambua mafanikio makubwa yaliyopatikana
nchini katika Nyanja mbalimbali kutokana na uongozi wake mahiri.
Rais Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akipeana mkono na Gavana wa Shirika la Lions Club
nchini Bwana Wilson Ndesanjo mara baada ya kuvalishwa medali maalum
ya Uongozi Bora na mahusiano mema wakati wa hafla fupi iliyofanyika
ikulu jijini Dar es Salaam leo
Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa klabu ya
Lions waliofika ikulu jijini Dar es Salaam leo kushiriki hafla ya
kumtunuku Rais Kikwete medali maalumu ya Uongozi Bora na Mahusiano
mema. (Picha na Freddy Maro).



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni