.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 16 Aprili 2014

MAADHIMISHO YA KUELEKEA MIAKA 50 YA MUUNGANO,MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA BANDA LA BUNGE


Afisa Habari wa Bunge Bw. Prosper Minja akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe, Dkt. Gharib Bilal (katikati) juu ya kazi mbalimbali zifanywazo na Ofisi ya Bunge wakati alipotembelea Banda la Bunge leo kwenye Maadhimisho ya kuelekea Miaka Hamsini ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mhe. Mohamed Aboud

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Asangye Bangu akitoa maelezo ya kina mbele ya Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe, Dkt. Gharib Bilal (katikati) kuhusu namna Bodi hiyo inavyofanya kazi katika kutoa mikopo kwa wanafunzi mbalimbali nchini mara alipotembelea Banda la Bodi ya Mikopo leo kwenye Maadhimisho ya kuelekea Miaka Hamsini ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel

Mhe. Mohamed Aboud akieleza jambo mbele ya waandishi wa habari (hawako pichani) waliohudhuria maonesho ya Maadhimisho ya kuelekea Miaka Hamsini ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

                                         PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni