.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 17 Aprili 2014

RAIS KIKWETE NA WANAFUNZI KATIKA PANTONI, AHANI KIFO CHA KADA WA CCM, APOKEA TUZO ALIYOTUNUKIWA MAREKANI


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru baada ya kupokea toka kwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe Tuzo ya Uongozi Bora Afrika aliyotuzwa nchini Marekani ambako aliwakilishwa na Mhe Membe

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea toka kwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe Tuzo ya Uongozi Bora Afrika aliyotuzwa nchini Marekani ambako aliwakilishwa na Mhe Membe

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, wakiangalia cheti cha heshima alichopewa na Gavana wa Maryland wakati wa kupokea Tuzo ya Uongozi Bora Afrika aliyotuzwa nchini Marekani ambako aliwakilishwa na Mhe Membe
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuhani na kutoa heshima za mwisho kwenye msiba wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada jijini Dar es salaam leo April 17, 2014 

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada jijini Dar es salaam leo April 17, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na watoto Samir Juma (fulana nyekundu) na Salum Chumu wakiwa katika pantoni la MV Magogoni wakivuka kuelekea Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 17, 2014. Watoto hao ambao wanasoma darasa la awali katika shule ya msingi ya Bunge, walipata bahati ya kuketi na baadaye kutelemka na Rais aliyekuwa akielekea kuhani msiba wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika Kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe wakiongea na watoto Samir Juma (fulana nyekundu) na Salum Chumu wakiwa katika pantoni la MV Magogoni wakivuka kuelekea Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 17, 2014. Watoto hao ambao wanasoma darasa la awali katika shule ya msingi ya Bunge, walipata bahati ya kuketi na viongozi hao waliokuwa wakielekea kuhani msiba wa kada wa CCM Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni