.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 15 Mei 2014

ABIRIA MLEVI AMFANYA RUBANI KUGEUZA WALIPOTOKA MUDA MFUPI BAADA YA NDEGE KUPAA

Abiria mmoja aliyekuwa anasafiri na ndege ya Shirika la Ndege la Marekani, U.S Airways kutoka Philadelphia kuelekea London Uingereza alimfanya rubani wa ndege hiyo kugeuza na kulazimika kutua tena Philadelphia muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutokana na abiria huyo kuwa kero kwa wahudumu wa ndege na abiria wenzake.
Abiria huyo Robert John Coppack mwenye miaka 40 aliyekuwa amelewa pombe, anashutumiwa kuwabughudhi wanawake wawili aliokuwa amekaa nao jirani, na hata wanawake hao walipoomba msaada kwa wahudumu wa ndege, bado abiria huyo aliendelea kuwa kero hata kwa wahudumu hao. Hatua hiyo iliwafanya wahudumu hao kuwasiliana na rubani ambaye alilazimika kugeuza ndege na kurejea tena Philadelphia.
Baada ya kushushwa kwa abiria huyo, ndege hiyo ilendelea na safari yake ya kuelekea London. Abiria huyo anaweza kuhukumiwa hadi kifungo cha miaka 20 jela akipatikana na hatia.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni