Mtu mmoja amefariki dunia baada ya gari lake kugonga treni ya abiria iendayo kasi katika kivuko cha treni huko Ivy Lea, Scampston karibu na Malton Kaskazini mwa Yorkshire.
Katika ajali hiyo, aliyepoteza maisha ambaye hakutajwa jina ana umri wa miaka 77 ambaye alikuwa dereva wa gari lililogongana na treni hiyo leo asubuhi.
Hakuna abiria aliyekuwa katika treni hiyo aliyeripotiwa kujeruhiwa, ila dereva wa treni hiyo anapatiwa matibabu baada ya kupata mshituko mkubwa baada ya ajali hiyo.
Sehemu ya mabaki ya gari hilo ikiwa imening'inia katika behewa la treni hiyo.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni