.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 5 Mei 2014

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR, MAALIM SEIF AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KATIKA MAZIKO YA SHEIKH ILUNGA


Maalim Seif akishiriki mazishi ya Sheikh Ilunga Hassan Kapungu katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni Dar es Salaam. Maelfu ya Waislamu wakijitokeza kumzika sheikh Ilunga.

                                                                  (Picha na Salmin Said, OMKR)

                                                                    Na. Hassan Hamad (OMKR).

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewaongoza maelfu ya waislamu katika mazishi ya sheikh maarufu wa Mkoa wa Mwanza na mwanaharakati wa dini ya Kiislamu marehemu sheikh Ilunga Hassan Kapungu.

Sheikh Ilunga amefariki dunia mjini Dar es Salaam na kuzikwa katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.

Katika uhai wake sheikh Ilunga Kapungu alikuwa mwanaharakati ambaye mara nyingi alikuwa akiendesha mihadhara ya wazi ya dini ya Kiislamu, ambapo mwishoni mwa mwaka 2013 alikamatwa kwa tuhuma za uchochezi mkoani Tabora na baadaye kuachiwa huru.

Kwa mujibu wa taarifa za kimtandao, kabla ya kukamatwa kwake na kuachiwa huru Disemba mwaka 2013, marehemu sheikh Ilunga alikwenda nchini India kwa matibabu baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo pamoja na sukari.
Akizungumza katika mazishi hayo sheikh Basaleh wa Dar es Salaam, amesema marehemu sheikh Ilunga alikuwa mwanaharakati imara na ni mfano mzuri wa kuigwa katika harakati za dini ya Kiislamu.
Mazishi yake yameweka historia baada ya maelfu ya waislamu kujitokeza kushiriki kwao, hali iliyopelekea mchanga wa kaburi lake kufukiwa kwa mikono badala ya kutumia mapauro na majembe kama ilivyozoeleka.
Masheikh kutoka Mikoa mbali mbali ya Tanzania wameshiriki mazishi hayo akiwemo sheikh Kishki, pamoja na wawakilishi wa Jumuiya ya Uamsho.







Hakuna maoni :

Chapisha Maoni