Mtaalam wa silaha ameigiza
jinsi Reeva Steenkamp alivyopigwa risasi na mpenzi wake Oscar
Pistorius, katika sehemua ya maelezo yake ya utetezi mahakamani
ambayo yalipelekea Pistorius kuchanganyikiwa kizimbani.
Afisa wa zamani wa polisi
Wollie Wolmarans aliigiza nafasi ya mwanamitindo huyo akiwa ndani ya
choo cha Pistorius akipigwa risasi siku ya tukio hilo la Februari 14
mwaka jana.
Akiwa nyuma ya mlango huo
aliigiza namna Steenkamp alivyokuwa akisimama chooni na kutaka
kufungua mlango wakati Pistorius akimpiga risasi na kufa.
Ushahidi huo unakinzana na
madai kuwa Pistorius alimpiga risasi Steenkamp baada ya kutokea
mabishano na kwenda kujifungia chooni ili kuepusha shari.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni