.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 8 Mei 2014

NSSF YATOA SEMINA KWA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO WA MADINI JIJINI MWANZA

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la taifa la Hifadhi ya jamii NSSF Crescentius Magori akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na NSSF kuhusu mfuko huo kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza.
Naibu waziri wa wizara ya Nishati na Madini nchini Steven Masele ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi akizindua Mpango maalum na kufungua Semina kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza.
"Serikali imetumia zaidi ya shilingi milioni 250 kuwakusanya wachimbaji wadogo ili waweze kuwa na vyama vyao, wapate kutambuliwa ili wapate kusaidiwa," kisha akaongeza Rais wa Shirikisho la wachimbaji madini Chama cha wachimbaji TZ (FEMATA) John Bina kwa kusema "Napenda kuwahakikishienikuwa kwa sasa wachimbaji wadogo tumejipanga, Ile dhana ambayo watanzania wengi wamekuwa nayo kuwa siye wachimbaji wadogo ni watu wa kutangatanga au wakuzurura haipo!"
Meneja kiongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii NSSF mkoa wa Mwanza akitoa maelezo ya awali na kutambulisha wadau mbalimbali walio hudhuria Semina kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza, ikiandaliwa na NSSF.
Naibu waziri Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Steven Masele, akipata picha ya pamoja na Viongozi wa NSSF pamoja na baadhi ya wanachama wa Chama cha wachimbaji wadogo wadogo wa madini (FEMATA).

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni