.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 7 Mei 2014

TASAF YAWAFUNDA WATAALAM WA KISEKTA JUU YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI-PSSN


Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akifungua warsha ya wataalam wa Kisekta (hawapo pichani) jijini Dar es salaam.


Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF Bwana Amadeus Kamagenge (aliyesimama)akitoa maelezo ya utangulizi katika warsha ya wataalamu wa kisekta jijini Dar es salaam katikati ni Mkurugenzi mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga na kushoto kwake ni mkurugenzi wa uratibu wa TASAF Alphonse Kyariga.

Mkurugenzi mtendaji wa TASAF, bwana Ladislaus Mwamanga amesema utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF utasisimua shughuli za maendeleo kwenye maeneo mbalimbali ya nchi ambako utatekelezwa na hivyo kuwa chachu ya maendeleo na kuondoa kero zinazowakabili wananchi hususani suala la umasikini.

Bwana Mwamanga amesema hayo jiji Dar es salaam alipofungua warsha ya wataalamu wa kisekta kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambao sekta zao zinahusika kwa namna moja au nyingine katika utekelezaji wa shughuli za TASAF kwenye maeneo yao.

Mkurugenzi mtendaji huyo wa TASAF amesema kwa kiwango kikubwa utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya masikini umeanza kutekelezwa kwa mafanikio ambapo mwelekeo umeonyesha kuwa maeneo ambako Mpango huo umefanyiwa majaribio kumekuwa na mafanikio ya kujivunia hususani katika sekta za Elimu, Afya, na hata Lishe kwa kaya ambazo hapo awali hazikuwa na uhakika wa kupata lishe.

Hata hivyo, bwana Mwamanga amewataka wataalamu hao wa kisekta kutumia utaalamu wao ipasavyo ili waweze kuielewa dhana nzima ya Mpango wa kunusuru kaya masikini na kuhakikisha kuwa wanawawezesha wananchi hususani walioko katika kaya masikini ili waweze kuondokana na umasikini.

Mkurugenzi huyo mtendaji wa TASAF pia ametaka mkakati maalum uwekwe ili kuhakikisha kuwa huduma muhimu hususani za upatikanaji wa elimu na Afya unakuwapo ili walengwa wa mpango huo waweze kunufaika nazo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni